Bendi ya Destiny's Child kuungana upya?

Destiny's Child
Image caption Destiny's Child

Akaunti mpya ya Instagram inayodaiwa kuwa ile ya kundi la Destiny's Child imebuniwa huku mashabiki wakitumai kwamba huenda kundi hilo likaungana tena.

Akaunti hiyo ambayo imethibitishwa ilionekana siku ya Jumamosi na sasa imechapisha picha za kusherehekea hatua iliopigwa na kundi hilo.

Wanachama watatu wa kundi hilo walitawanyika mwaka 2006 lakini mwaka ujao bendi hiyo itaadhimisha miaka 20.

Hatahivyo mashabiki wameanza kuzua uvumi kuhusu umuhimu wa akaunti hiyo katika siku zijazo.

Akaunti hiyo imefuatwa na takriban mashabiki 12,000 wote wakitaka wanachama wa kundi hilo kufanya ziara ya muungano mpya.

Wanachama wa bendi hiyo ni Kelly Rowland,Michelle Williams na Beyonce.