Saudia yazima njama ya ulipuaji wa mechi ya kombe la dunia

Saudia ilitarajiwa kucheza dhidi ya muungano wa milki za kiarabu mnamo mwezi Oktoba
Image caption Saudia ilitarajiwa kucheza dhidi ya muungano wa milki za kiarabu mnamo mwezi Oktoba

Saudia imetibua mpango wa kulipua mechi ya kimataifa ya soka katika uwanja wa mji uliopo magharibi mwa taifa hilo Jeddah.

Wapiganaji walikuwa wamepanga kulipua mechi hiyo ya kufuzu kombe la dunia kati ya Saudia na muungano wa milki za kiarabu UAE kupitia gari lililojazwa vilipuzi mnamo mwezi Oktoba.

Mamlaka inasema kuwa imetibua jaribio la pili ililopangwa na Islamic state kuwaua maafisa wa usalama karibu na Riyadh.

Washukiwa wanane wamekamatwa kutoka kwa maficho yao,maafisa wamesema.

Kati yao ni raia wa Saudia ,raia 2 wa Pakistan,raia mmoja wa Syria pamoja na mwengine wa Sudan kulingana na wizara ya maswala ya ndani.