Italia: Maelfu ya wakazi walala nje kufuatia tetemeko

Nyumba zimeharibiwa vibaya
Image caption Nyumba zimeharibiwa vibaya

Maelfu ya watu katikati mwa Italia wamelala katika magari na mahema ikiwa ni kama makazi ya muda mfupi baada ya tetemeko kubwa kupiga katika eneo hilo tokea kile cha mwezi Agosti.

Wakaazi katika eneo lililoathirika zaidi la Norcia wamesema walikuwa na hofu sana kuendelea kukaa ndani mwa nyumba zao.

Takriban watu 20 wamejeruhiwa na tetemeko hilo lililotokea siku ya Jumapili, lakini inasemekana mtu mmoja amepoteza maisha.

Image caption Baadhi ya wakaazi wakiwa kwenye makazi ya muda

Mkuu wa eneo hilo Luca Ceriscioli amesema zaidi ya watu laki moja watahitaji msaada.