Mchungaji achaguliwa meya wa Rio de Janeiro, Brazil

Rais Michel Temer amesifia uchaguzi huo
Image caption Rais Michel Temer amesifia uchaguzi huo

Mchungaji wa kanisa la kiinjili amechaguliwa kuwa meya wa jiji la Rio de Janeiro.

Marcelo Crivella ambaye ni mpwa wa mwanzilishi wa kanila la kiinjili la megachurch amekuwa akilalamikiwa kwa kuhusishwa kushiririki katika mapenzi ya jinsia moja.

Alishinda kwa zaidi ya asilimia 20 katika uchaguzi wa mzunguko wa pili wa manispaa akimshinda Marcelo Freixo wa mrengo wa kushoto.

Rais wa nchi hiyo Michel Temer amesifia uchaguzi huo na kusema ulikuwa wa huru na haki na aliyepaswa kushinda ameibuka mshindi.

Ushindi wake kajika mji huo wa pili kwa ukubwa nchini Brazil, unamaanisha kuongezeka kwa wapiga kura wa kanisa hilo na mabadiliko kuelekea mrengo wa kulia wa siasa za mji wa Rio.