'Diwali' yalaumiwa kuchafua hewa mjini Delhi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Barabara Kuu mjini Delhi,

Wakaazi wa jiji kuu la India, Delhi wameghathabishwa na kile wamesema kuwepo ukungu mkubwa uliosababishwa na fataki nyingi zilizorushwa katika sherehe za Diwali.

Mamlaka zilionya uchafuzi wa hewa kutokana na fataki hizo kutumiwa juu ya kiwango kilichowekwa. Sherehe za Diwali ni muhimu sana katika imani ya Kihindi na huadhimisha ushindi wa wema dhidi ya ubaya.

Baraza la mji wa Delhi liliahidi kuweka vifaa muhimu za kusafisha hewa wakati wa sherehe hizo. Kabla ya Diwali kumekua na kampeini kadhaa zikiwataka raia kutofyatua fataki. Hata hivyo wito huo haikutiliwa maanani. Urushaji wa fataki huambatana na sherehe za Diwali na wengi huona hii kama ishara ya utajiri.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ukungu wafunika mji wa Delhi, India

Familia na kampuni za biashara nchini India hutumia maelfu ya dola kununua fataki ambazo hurushwa usiku wakati wa sherehe hizo. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani{WHO} miji 13 kati ya 20 ambayo imechafuliwa zaidi duniani inapatikana India.

Kando na fataki, India pia huchafuliwa hewa wakati wa msimu wa baridi ambapo jamii masikini hulazimika kuchoma takataka kama njiya ya kupata joto hususan wakati wa usiku. Aidha kuna desturi ya kuchoma mashamba baada ya mavuno na moto huchukua siku kadhaa kabla ya kuzima