Vikosi vya Iraq vyakaribia kuudhibiti mji wa Mosul

Vikosi vya uokoaji vikisaidia wahanga
Image caption Vikosi vya uokoaji vikisaidia wahanga

Vikosi vya Iraq sasa vimebaki kilomita moja tu kudhibiti mji wa Mosul, mji wa mwisho kwa ukubwa nchini humo bado unadhibitiwa na wapiganaji wa Islamic State.

Vikosi maalum vinaelekea katika mji wa Mosul kutoka Mashariki walifanya mashambulizi kabla ya alfajiri.

Image caption Maeneo yaliyozingirwa na vikosi vya Iraq

Mwandishi wa BBC anayesafiri na safu ya kivita alisema wamekuwa wakilengwa mara kwa mara na wapiganaji wa kundi la IS waliokuwa wakiendesha magari yaliotegeshwa mabomu.

Lakini bado mafanikio ni makubwa na vikosi vya serikali vimesonga mbele hadi kijiji cha Bazwaya, nje kidogo ya mji wa Mosul.