Theresa May aunga mkono gavana wa benki kuu kusalia kazini

Theresa ameingia madarakani Julai 2016
Image caption Theresa ameingia madarakani Julai 2016

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ameunga mkono wazo la gavana wa benki kuu ya Uingereza la kusalia katika kazi yake kwa mwaka mmoja zaidi.

Mark Carney amesema kuwa atasalia mpaka mwezi June 2019 kusaidia kuimarisha uchumi wakati huu ambao Uingereza inamalizia taratibu zake za kujitoa ndani ya umoja wa Ulaya baada ya kupiga kura ya kujiondoa.

Image caption Mark Carney

Tangazo lake limeondoa wasiwasi juu ya mustakabali wake katika kazi hiyo.

Carney amekuwa akikosolewa na wanasiasa waliounga mkono kujiondoa kwenye umoja wa Ulaya kwa kitendo chake kwa kueleza kuwa patakotea matatizo ya kiuchumi iwapo Uingereza itafanya hivyo.