Magufuli: Huwa nawasiliana na Rais Kenyatta

Magufuli: Huwa nawasiliana na Rais Kenyatta

Baada ya mwaka mzima tangu kuchaguliwa, rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amefanya ziara ya kwanza ya kiserikali nchini Kenya.

Kulikuwepo uvumi kuwa huenda kuna tofauti kali ya rais huyo na mwenzake wa Kenya hasa baada ya rais Magufuli kukosa kuhudhuria mkutano mkuu wa kibiashara ulioandaliwa jijini Nairobi.

Ziara hiyo ya siku mbili inanuiwa kudhihirisha nia safi kati ya Kenya na Tanzania pamoja na kuimarisha biashara.

Dayo Yusuf na taaifa hii kutoka Nairobi.