Simu zatumiwa kukusanya maelezo ya kuzaliwa Tanzania

Simu zatumiwa kukusanya maelezo ya kuzaliwa Tanzania

Nchi za Afrika kusini mwa jangwa la Sahara zinakumbwa na changamoto ya kupanga mipango ya maendeleo kutokana na ukosefu wa taarifa rasmi za watu wake.

Nchini Tanzania kwa mfano, zaidi ya asilimia 80 ya raia wa nchi hiyo hawana vyeti vya kuzaliwa- hii ni kwa mujibu wa taasisi ya serikali ya kuandikisha watu- RITA.

Ili kukabiliana na tatizo hilo, serikali ya Tanzania imeanzisha utaratibu wa kukusanya taarifa muhimu za kuzaliwa kwa kutumia teknolojia ya simu za mkononi.

Mwandishi wetu Sammy Awami amefuatilia zaidi taarifa hii kutoka Mwanza, Tanzania.