Mboga ya mchicha kugundua bomu

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mboga ya Spinach kugundua bomu iliyotegwa arthini

Wanasayansi wameweza kuifanya mboga ya aina ya Mchicha au 'Spinach' kugundua bomu.

Imearifiwa kwamba majani ya mchicha yanaweza kuhifadhi kemikali aina ya 'nitro-aromatics' ambazo hupatikana kwenye mabomu ya kutegwa arthini na silaha zinazozikwa arthini.

Siyo lazima mboga hii iwekwe nyaya yeyote ili kuweza kugundua bomu, bali mmoja anaweza kufahamu kwa kutizama au kwa taarifa maalum za simu.Utafiti huu umefanikishwa na Chuo Ki Kuu cha Massachusetts Institute of Technology-MIT.

Haki miliki ya picha MIN HAO WONG
Image caption Boga hiyo ya Spinacha itafanyiwa uchunguzi zaidi

Wanasayansi waliweka kemikali za carboni kwenye maji na kisha kufanya mizizi ya mboga kupitisha maji yale hadi kwenye matawi ya mchicha. Kisha wanasayansi wakapapasa majani ya mchicha na vyuma maalum.Majani yale yalianza kutoa chembechembe za moto ambazo zinaweza kuonekana kwa kopyuta.

Pia chembechembe hizo zinaweza kuonekana kwa simu ya mkononi. Wanasayansi sasa wanasema mboga ya mchicha pia inaweza kutumika kufahamu uwepo wa visima vya maji arthini, kemikali zilizovuja kutoka kwa silaha na madini ya nitro-aromatics. kwa sasa wananuia kuwezesha mboga hiyo kuweza kugundua bomu iliyotegwaa arthini kwa kwa mbali.