Agonga gari la polisi akijipiga selfie

Miranda Radar aligonga gari la polisi huku akijipiga selfie Haki miliki ya picha BRYAN POLICE DEPARTMENT
Image caption Miranda Radar aligonga gari la polisi huku akijipiga selfie

Mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu nchini Marekani aligongesha gari lake kwa lile la polisi, wakati akijipiga picha za selfie huku akiendesha gari.

Miranda Rader mwenye umri wa miaka 19, aligonga gari polisi alipokuwa akimtumia mpenzi wake picha za utupu kupitia kwa mtandao wa Snapchat.

Ajali hiyo iliyotokea eneo la Bryan umbali wa kilomita 160 Kaskazini mwa mji wa Houston, ilisababisha mfuko wa hewa kuchomoka

Mwanafunzi huyo pia alipatikana na chupa ya mvinyo ndani ya gari lake kwa mujibu wa polisi. Hakuna mtu aliyejeruhiwa.

Polisi ambaye gari lake liligongwa alikaribia gari la Bi Rader na kumpata akijaribu kuvaa nguo. Alipoulizwa mbona, alijibu akisema kuwa alikuwa akijipiga picha za selfie za kumtumia mpenzi wake.

Alikamatwa kwa kushukiwa kuendesha gari akiwa mlevi na kuachiliwa kwa dhamana ya dola 2000.