Marekani yaiongezea Sudan muda wa vikwazo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Marekani inasema kuwa Sudan ni tisho kwa usalama wake

Serikali ya Marekani imeongeza muda wa vikwazo dhidi ya Sudan kwa mwaka mmoja zaidi, ikisema kuwa Sudan imesalia kuwa nchi hatari kwa usalama wake kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

"Vitendo na sera za serikali ya Sudan vinaendelea kuwa tisho kwa usalama wetu na kwa sera za kigeni za Mareknai," ilisema taarifa ya Rais Barack Obama.

Sudan iliwekewa vikwazo vya kibiashara na Marekania tangu mwaka 1997, kwa madai kuwa inaunga mkono makundi ya kigaidi.