Wanajeshi wa Iraq waingia Mosul

Karibu wanajeshi 50,000 wanaelekea Mosul
Image caption Karibu wanajeshi 50,000 wanaelekea Mosul

Vikosi vya jeshi la Iraq kwa mara ya kwanza kabisa vimeingia maeneo ya mashariki mwa mji wa Mosul wakati wanajaribu kuwatimua wanamgambo wa Islamic State kutoka mji huo ulio Kaskazini mwa nchi.

Vikosi maalum vya kupambana na ugaidi vilichukua udhibiti wa jengo la runinga ya taifa eneo la Kukjali saa kadha baada ya kufanya mashambulizi eneo hilo.

Lakini mwandishi wa bbc anayeandamana na vikosi hivyo anasema kuwa wanakabiliwa na upinzani mkali.

Haki miliki ya picha @BBCIPANNELL
Image caption Vikosi maalum vya Iraq vilikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa ISIS

Siku ya Jumatatu waziri mkuu wa Iraq Haider al-Abadi, aliwaambia wanamgambo 3000 na 5000 walio ndani ya mji wa Mosul baaada ya kuuteka mwezi Juni mwaka 2014, kuwa hakuna njia ya kukimbia kwa hivyo ni afadhali wasalimu amri au wafe.

Karibu wanajeshi 50,000 wa Iraq, wapiganaji wa kurdi na wale kutoka Sunni na Shia wanashiriki kwenye mapigano hayo ya wiki mbili, kuwatimua Islamic State kutoka ngome ya kuu na ya mwisho nchini Iraq.

Haki miliki ya picha @FERASKILANIBBC
Image caption Vikosi vya Iraq vinataka kuwa na ngome ndani ya Mosul

Vikosi hivyo vilichukua udhibiti wa kijiji cha Bazwaya kilicho mashariki mwa Mosul siku ya Jumatatu kaala ya kuelekea eneo la viwanda la Kukjali.

Ikiwa vikosi hivyo vitakuwa na ngome ndani ya mji wa Mosul, itakuwa mafanikio makubwa kwa Iraq na nchi zingine zote ambazo zimeshiriki kwenye vita dhidi ya kundi la Islamic State.