Makurutu bandia wa jeshi wakamatwa Kenya

Jeshi la Kenya huwapa ajira vijana kwenye nchi yenye ukosefu mkubwa wa ajira Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jeshi la Kenya huwapa ajira vijana kwenye nchi yenye ukosefu mkubwa wa ajira

Watu kadha wamekamatwa kwenye kambi ya kijeshi nchini Kenya baada ya kuwasili na barua bandia za kujiunga na jeshi.

Utawala unasema kuwa watu hao 57 walikamatwa walipowasili kwenye shule ya makurutu katika kambi ya Moi iliyo mjini Eldoret, wakiwa miongoni mwa wale waliokuwa na barua halali za kujiunga na jeshi.

Wale wote waliokamatwa walikuwa na barua za kuwajulisha kuripoti kambini tarehe 31 mwezi Oktoba, baada ya zoezo lililodumu mwezi mzima la kuwatafuta watu wa kujiunga na jeshi.

Idara ya ujasusi nchini Kenya inasema inashirikiana na jeshi kubaini ni wapi barua hizo zilitoka.