Buhari akutana na viongozi wa Niger Delta

Image caption Baadhi ya viongozi kutoka eneo la Niger Delta

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, amekutana na viongozi kutoka maeneo ya Niger Delta, katika harakati za kumaliza mashambulio ya mara kwa mara kutoka kwa wanamgambo wa kiislamu, dhidi ya vifaa vya mafuta katika eneo hilo.

Waakilishi wa wanamgambo hao waliripotiwa kuwa miongoni mwa wajumbe katika mazungumzo yaliyofanyika katika mji mkuu Abuja.

Mwandishi wa BBC anasema kuhusika moja kwa moja kwa bwana buhari katika mazungzoa hayo, ni hatua dhahiri kuwa anataka kutanzua mzozo huo.

Ghasia katika maeneo hayo, zimepunguza pakubwa uzalishji wa mafuta hatua iliyo athiri uchumi wa Nigeria , taifa tajiri barani Afrika.,

Makundi ya wapiganaji yanadai kuwa yanapigana ili serikali iwape wenyeji wa maeneo hayo mgao unaostahili wa mapato ya mafuta yanayotoka sehemu hiyo.

Hata hivyo serikali inawalaumu kwa kuitatiza nchi.