Ndege zashambulia mji wa Qandala nchini Somalia

Kundi kutoka kwa wapiganaji wa al-Shabab eneo la Puntland lilitangaza kulitii Islamic State.
Image caption Kundi kutoka kwa wapiganaji wa al-Shabab eneo la Puntland lilitangaza kulitii Islamic State.

Ndege zisizojulikana zimefanya mashambulizi katika mji wa Qandala ulio Kaskazini mwa Somalia ambao unadhibitiwa na Islamic State.

Kundi dogo la wapiganaji walio watiifu kwa Islamic Sate waliteka mji huo mdogo ulio eneo linalojisimamia la Puntlaand wiki iliyopita.

Vyombo vya habari nchini Somalia vilisema kuwa wapiganaji hao waliondoka mji huo chini ya saa 24 baada ya kuuteka, lakini kamishna wa wilaya ya Qandala ambate aliukimbia mji huo akasema kuwa kundi bado linaudhibiti.

Mwaka mmoja uliopita kundi kutoka kwa wapiganaji wa al-Shabab eneo la Puntland lilitangaza kulitii Islamic State.

Kundi hilo lililojitenga linaongozwa na Abdikadir Mumin, ambaye aliwekewa vikwazo na Marekani mwezi uliopita kutoka na kile Marekani inakitaja kuwa kuhusika na ugaidi.