UN yakiri vikosi vyake kushindwa kuwalinda raia Sudani Kusini

UN ina walinda amani 16,000 Sudani Kusini
Image caption UN ina walinda amani 16,000 Sudani Kusini

Umoja wa mataifa imekiri kuwa vikosi vyake vya kulinda Amani Sudani Kusini vimeshindwa kuwalinda raia katika mji mkuu wa Juba wakati wa mapigono baina ya pande mbili mwezi Julai.

Afisa wa kulinda amani Aditya Mehta amesema kwamba wakati kukiwa na wasiwasi kidogo kuwa vikosi vya umoja wa mataifa vimesaidia kuokoa maisha ya mamia kati ya maelfu ya raia wa Sudan Kusini, imebainika kwamba ilihitajika kurejesha amani ya jamii zisizo na ulinzi.

Mapema, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- Moon alimtimua kamanda wa kikosi cha kulinda amani baada ya utafiti wa ndani kubaini kuwa vikosi vya kulinda amani vilikataa kujibu mashambulizi wakati wanajeshi wa serikali walipowashambulia wafanyakazi wa mashirika ya kigeni ya misaada.