UN: IS wanatekeleza mauaji zaidi kwa wa Iraq

UN Imetoa angalizo kwa vikosi vya serikali ya Iraq kuwa makini wanapo walenga wapiganaji hao
Image caption UN Imetoa angalizo kwa vikosi vya serikali ya Iraq kuwa makini wanapo walenga wapiganaji hao

Umoja wa mataifa umesema , umepokea taarifa za kuwepo kwa mauaji zaidi na utekaji uliotekelezwa na wapiganaji wa Islamic State kusini mwa mji Mosul nchini Iraq.

Siku ya jumamosi waliokuwa wafanyakazi wa vikosi vya serikali waliuawa.

Msemaji wa idara ya haki za binadamu wa umoja wa mataifa Kwa mjibu wa umoja wa mataifa, Ravina Shadasani anasema kuwa IS wanadaiwa kuwatumia raia kama ngao yao katika eneo la mapigano, ambapo wamejaribu kuwahamisha raia wapatao 25,000 kutoka mji jirani na Masul na kuwafanya ngome yao.

Kutokana na mbinu hizo za IS, UN Imetoa angalizo kwa vikosi vya serikali ya Iraq kuwa makini wanapo walenga wapiganaji hao, ili kutosababisha madhara kwa raia wa kawaida.

Vikosi vya serikali ya Iraq, kwa sasa vinaendeleza jitihada za kuukomboa mji wa Mosul kutoka mikononi mwa IS.