Polisi wamkamata mtu aliyeshukiwa kuwaua polisi Marekani

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mshukiwa huyo anatajwa kuwa Scott Michael Greene

Polisi katika jimbo la Iowa nchini Marekani, wamesema kwamba wamemkamata mshukiwa mmoja baada ya kuuwawa kwa maafisa wawili wa polisi kwa kupigwa risasi.

Awali polisi walitangaza kuwa walikuwa wakimtafuta Scott Michael Greene, mwanamme mzungu mwenye umri wa miaka 46 kutoka eneo la Urbandale, kufuatia kumtaja kuwa mshukiwa.

Polisi wa kwanza alipatikana akiwa amepigwa risasi eneo la Urbandale mwend wa saa saba usiku saa za marekani siku ya Jumatano. Polisi wa pili naye alipatikana dakika ishirini baadaye hatua chache.

Wote hao walikuwa wameketi ndani ya magari yao wakati walishambuliwa. Lengo la mauaji hayo bado halijulikani.

Shule zote eneo la Urbandale ziliesalia zimefungwa leo Jumatano kufuatia ushauri wa polisi.