Amnesty International: Wapiganaji wa Kisuni wanashiriki vita Mosul

Wapiganaji kutoka kabila lenye nguvu wamekuwa wakimshambulia yoyote ambaye wanaamini kuwa ana uhusiano na IS
Image caption Wapiganaji kutoka kabila lenye nguvu wamekuwa wakimshambulia yoyote ambaye wanaamini kuwa ana uhusiano na IS

Shirika la haki za binaadamu, Amnesty international, linasema kuwa kuna ushahidi mkubwa kwamba wapiganaji wa kisuni wanasaidia katika kampeni za kuukomboa mji wa Mosul kutoka mikononi mwa Islamic State.

Wamekuwa wakilipa kisasi dhidi ya wakazi wa mji huo huku watoto wadogo wakishukiwa kuwaunga mkono wapiganaji wa IS.

Ripoti ya shuhuda mmoja inasema kuwa wapiganaji kutoka kabila lenye nguvu wamekuwa wakimshambulia yoyote ambaye wanaamini kuwa ana uhusiano na IS katika vijiji vilivyokombolewa kusini Mashariki mwa Mosul.

Chanzo kutoka eneo hilo kililiambia shirika la haki za binadam kuwa wameona watu wakipigwa, wakipigwa shoti za umeme muda mwingine wakiburuzwa kwa gari mitaani.

Nje kidogo Mashariki mwa Mosul, wanajeshi wa Iraq wanafanya msako wa nyumba hadi nyumba kuona kama kuna mpiganaji yeyote wa IS aliyesalia.