Kiongozi wa Iran adharau mwenendo wa kampeni za Marekani

Uchaguzi wa Marekani utafanyika siku ya Jumanne ya Novemba 8, 2016
Maelezo ya picha,

Uchaguzi wa Marekani utafanyika siku ya Jumanne ya Novemba 8, 2016

Kiongozi mkuu wa Irani Ayatollah Ali Khamenei, amedharau mwenendo wa kampeni za urais Marekani.

Amesema kuwa matamshi ya wagombea wote wawili wakati wa midahalo yote ni ushahidi wa uvunjifu wa thamani ya binadamu nchini Marekani.

Ameonya kudhibiti siasa nchini Iran dhidi ya makubaliano ya moja kwa moja na Marekani kwa jambo lolote.

Katika hotuba tofauti Rais Hassan Rouhani ameelezea kuwa chaguo lililombele ya raia wa Marekani kuwa ni baya na chafu.

Na aliyekuwa Rais wan nchi hiyo Akbar Hashemi Rafsanjani amemuelezea Donald Trump kuwa ni mtu hatari.

Wairani wanaona kwamba kama Trump atashinda basi itakuwa ni vilio kuhusu makubaliano ya Nuklia na nchi zenye nguvu duniani, na kuanzishwa tena kwa vikwazo.