Obama aonya uchunguzi juu ya barua pepe za Clinton usiendeshwe kikashfa

Image caption Obama amemwaambia waandishi kwamba ana imani kamili juu ya mgombea urais wa Democratic.

Rais wa Marekani Barack Obama ameonya kuwa uchunguzi wa shirika la kijasusi la FBI kuhusu barua pepe za Hillary Clinton usiendeshwe kikashfa.

Obama amemwaambia waandishi wa Marekani kwamba anaimani kamili juu ya mgombea urais wa Democratic.

Maneno ya Obama yanaonekana kama ukosoaji usio wa wazi wazi kwa mkurugenzi wa shirika la upelelezi la FBI, James Comey, ambaye alitangaza wiki iliyopita kuwa shirika hilo limeanza tena uchunguzi baada ya kupokea barua pepe ambazo zinaweza kuwa za muhimu.

Bi Clinton amefanya ziara ya kushtukiza ya kampeni katika viwanja vya Florida leo Jumatano.

Donald Trump amabye pia yupo jimbo la Florida aliiambia hadhira kuwa lengo lake kubwa kama atakuwa rais ni kuridisha ajira. Bi Clinton badae ataenda kwenye majimbo ya Nevada na Arizona.