Pacha walioshikana watenganishwa hospitali ya Kenyatta
Huwezi kusikiliza tena

Pacha walioshikana watenganishwa hospitali ya Kenyatta

Madaktari nchini Kenya wamefanikiwa kufanya upasuaji wa kuwatenganisha pacha walioungana katika sehemu ya chini ya mgongo.

Pacha hao walikuwa hospitalini kwa muda wa miaka miwili tangu walipozaliwa wakingoja upasuaji wa kuwatenganisha.

Walizaliwa mwaka wa 2014 wakiwa na viungo vyote vya mwili isipokuwa sehemu ya chini ya uti wa mgongo ulioshikana na kuwasababisha kutumia njia moja kuenda haja kubwa.

Upasuaji wa aina hiyo kutenganisha sehemu ya uti wa mgongo ndio wa kwanza kufanyika katika eneo la kusini mwa Jangwa la Sahara.

Mwandishi wa BBC David Wafula na taarifa zaidi.