Je, unalingana vipi na viongozi mbalimbali duniani?

Marekani inapojiandaa kumchagua kiongozi mpya, Unajilinganisha vipi na watu wenye ushawishi mkubwa duniani? Je una elimu zaidi yao? Na umri je - wewe ni mdogo kuwaliko au umewazidi kwa umri? Una uzoefu mwingi kazini?

Fahamu jinsi unavyolingana na viongozi 195 duniani kulingana na data iliyokusanywa na BBC Monitoring.

Umri

Elimu

Muda kazini

Mfumo uliotumiwa

Data ya umri, elimu na muda ambao wamehudumu viongozi wa nchi 195 ilikusanywa na BBC Monitoring na mara ya mwisho kubadilishwa ilikuwa 15 Septemba 2016.

Viongozi ambao tarehe ya kuzaliwa kwao na kiwango chao cha elimu havipatikani hawakujumuishwa.

Kwa mradi huu, kiongozi wa nchi alifafanuliwa kama tu aliye na nguvu zaidi katika nchi.

Kwa San Marino, ambako kuna viongozi wawili wa taifa walio na mamlaka sawa na wanaohudumu kwa wakati mmoja, mmoja alichaguliwa pasi na kufuata utaratibu wowote.

Kwa wakati mwingi, tarehe aliyoapishwa kiongozi au alipopokea madaraka inachukuliwa ndio mwanzo wa muda wake madarakani.

Waliochangia

Imeandaliwa na Nassos Stylianou, Ed Lowther, Elisabetta Tollardo na John Walton. Utafiti wa data ulifanywa na kundi la watafiti wa BBC Monitoring Research. Usanifu ulifanywa na Tom Nurse, Gerry Fletcher na Zoe Bartholomew. Waandalizi wa kiufundi Steven Connor na Becky Rush.