Kenyatta: Tuna haki kuondoa majeshi Sudan Kusini

Rais Kenyatta ametetea hatua ya Kenya ya kuondoa wanajeshi wake kutoka Sudan Kusini Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais Kenyatta ametetea hatua ya Kenya ya kuondoa wanajeshi wake kutoka Sudan Kusini

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametetea hatua ya nchi yake na kuwaondoa wanajeshi wake kutoka kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani nchini Sudan Kusini.

Rais Kenyatta alisema kuwa Kenya imejitolea katika kuchangia amani katika kanda hii na dunia nzima lakini akaongeza kuwa heshima ya nchi haiwezi kuchafuliwa.

Bwana Kenyatta alikuwa akizungumza wakati aliongoza hafla ya kufuzu kwa wanajeshi kwenye chuo cha kutoa mafunzo ya kijeshi cha Lanet kaunti ya Nakuru.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ban ki-Moon alimuachisha kazi kamanda wa UN nchini Sudan Kusini ambaye anatoka Kenya

Alisema kuwa uamuzi wa kuondoka kwenye mpango huo wa amani, unafuatia visa vinavyaokua ujumbe wa umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini, ambapo Umoja wa Mataifa ulimlaumu kamada kutoka nchini Kenya.

Kenyatta aliongeza pia kuwa Kenya ina mpamgo ya kuwaondoa wanajeshi wake kutoka ujumbe huo ambao alisema umeanza kuwalaumu wakenya.

Kenyatta alisema kuwa kenya imachangia makanda wenye tajriba ya juu katika masuala ya kulinda amani wakiwemo Luteni Jenerali Daniel Opande ambaye alikuwa kamanda wa kikosi cha kulinda amanai nchini Sierra Leone na Luteni Jenerali Ngondi ambaye alikuwa kamanda nchini Liberia miongoni mwa wengine.