Zaidi ya wahamiaji 239 wafa baharini pwani ya Libya

Mashua mara nyingi hubeba wahamiaji wengi zaidi Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mashua mara nyingi hubeba wahamiaji wengi zaidi

Zaidi ya wahamiaji 239 wanaaminika kufa maji walipokuwa wakisafiri wakitumia mashua mbili pwani ya Libya.

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR lilifahamishwa kuhusu mkasa huo na manusura wawili waliopelekwa katika kisiwa cha Lampedusa

Hakuna maiti zilizopatikana hadi sasa.

Zaidi ya wahamiaji 4200 wamekufa wanapojariba kufanya safari hatari kuvuka bahari ya Mediterranean mwaka huu.

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa mwaka huu wa 2016 ndio utakuwa wenye vifo vingi zaidi vya wahamiaji.

Karibu wahamiaji 330,000 wamevuka bahari mwaka huu ikilinganishwa na zaidi ya wahamiaji milioni moja mwaka 2015.