Europa: Man U yachapwa ugenini

Image caption Aritz Aduriz

Michuano ya Ligi ya Europa iliendelea usiku wa kuamkia leo kwa michezo kadhaa kupigwa, Manchester United imekubali kichapo cha 2-1 kutoka kwa wenyeji wao Fenerbahçe ambapo meneja wa timu hiyo Jose Mourinho amesema timu yake ilicheza kama watalii, Athletic Bilbao ya Uhispania ikaichakaza KRC Genk ya Ubelgiji kwa bao 5-3 magoli yote ya Bilbao yakiwekwa kimiani na mshambuliaji Aritz Aduriz.

Image caption Manchester United wameshinda michezo miwili tu kati ya saba ya michuano yote

Matokeo ya michezo mingine

Zorya Luhansk 1-1 Feyenoord

FC Astana 1-1 Olympiakos

Apoel Nic 1-0 BSC Young Boys

FK Qabala 1-2 Saint-Étienne

Anderlecht 6-1 FSV Mainz 05

Maccabi Tel-Aviv 0-0 AZ Alkmaar Full time

Zenit St P 2-1 Dundalk

Astra Giurgiu 1-1 Viktoria Plzen

Austria Vienna 2-4 Roma

Sassuolo 2-2 Rapid Vienn