Polisi watumia mabomu ya machozi kuvunja maandamano Nairobi
Huwezi kusikiliza tena

Polisi watumia mabomu ya machozi kuvunja maandamano Nairobi

Polisi nchini Kenya Alhamisi walitumia mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha kuwatawanya waandamanaji mjini Nairobi wakipinga ufisadi.

Baadhi ya watu walipigwa kwa virungu na wengine kukamatwa. Waandamanaji wengi walivaa nguo nyekundu kama ishara ya kupinga kashfa ya hivi karibuni ya ufisadi iliyoikumba serikali ya Kenya.

Maafisa katika wizara ya Afya wanatuhumiwa kuiba dola za Kimarekani milioni hamsini zilizokuwa za mradi wa uzazi.