Uzito wa dini katika kampeni za uchaguzi Marekani

Uzito wa dini katika kampeni za uchaguzi Marekani

Dini ni ngumu kuitenganisha na siasa hapa Marekani. Wamarekani wengi wamekuwa wakisistiza kwamba ni muhimu kwao, Rais kuwa na imani sana ya dini.

Lakini uchaguzi huu umeshuhudia dini ikiwa na nafasi kubwa zaidi, huku Wamarekani wengi wakionyesha hasira zao dhidi ya vitisho vinavyotolewa na mgombea urais kupitia chama cha Republican Donald Trump ya kuwapiga marufuku Waislamu kuingia Marekani.

Kwa upande mwengine, Hillary Clinton, ameonya kuhusu kuwadharau Waislamu.

Kwa hiyo dini ina nguvu kiasi gani kwenye uchaguzi huu?

Zuhura Yunus amekutana na Wakristo na Waislamu wa Kiafrika katika jimbo la Michigan