Zaidi ya shule 60 kufungwa Uganda

Shirika la Bridge International lilifungua shule yake ya kwanza nchini Uganda mwaka 2015
Image caption Shirika la Bridge International lilifungua shule yake ya kwanza nchini Uganda mwaka 2015

Mahakama ya juu zaidi nchini Uganda imetoa amri kuwa zaidi ya shule 60 za msingi zinazosimamiwa na shirika la Bridge International Academies zifungwe.

Shirika hilo kutoka Marekani linasema kwa linatoa elimu ya gharama ya chini lakini yenye viwango vya juu kwa watoto maskini, ambayo inaungwa mkono na serikali ya Uingereza akiwemo mfanyibiashara tajiri Bill Gates na pia mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg.

Lakini shule hizo zimekumbwa na shutuma zikiwemo hali duni ya mazingira, ukosefu wa vifaa na kukosa kufuata mfuma wa elimu nchi humo.

Afisa mmoja wa wizara ya elimu anasema kuwa shule hizo zitafungwa mara moja hatua ambayo itaawaathiri wanafunzi 12,000 kati kati mwa muhula wa masomo.

Shirika la Bridge International ambalo lilifungua shule yake ya kwanza nchini Uganda mwaka 2015 linapinga uamuzi huo na kusema kuwa litaupinga.

Bridge Intenational pia hutoa huduma zake nchini India na Nigeria na mwezi Januari liliingia katika makubaliano na serikali ya Liberia kusimamia shule zake za msingi.