Huawei yazindua simu mpya ya Mate 9

Haki miliki ya picha HUAWEI
Image caption Huawei Mate 9

Huawei imezindua simu mpya yenye skrini kubwa wakati huu ambapo simu ya Samsung Galaxy Note 7 inakumbwa na changamoto.

Simu hiyo kwa jina Mate 9, ni kati ya simu za kwanza zinazotumia teknolojia ya Android 7 na inakuja ikiwa katika aina mbili za kamera.

Kampuni hiyo ya China inasema kuwa imeshughulikia tatizo la simu hizo kupoteza mauzo baadaye.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Sumsang ilisitisha uzalishaji wa simu ya Galaxy Note 7 kufuatia visa vya kuwaka moto

Lakini mtaalamu mmoja anasema kuwa wateja bado wanazitilia shaka simu za kampuni hiyo.

Simu za Huawei hazijafikia viwango vya simu za Samsung na ndiyo sababu huwa inafanya ushirikiano na kampuni zingine kama Leica na Porsche kuboresha teknolojia yake ya Kamera.

Samsung ilitizisha uundaji wa simu ya Note 7 mwezi uliopita baada ya simu kadha kuwaka moto.