Viongozi wa upinzani wakamatwa Uturuki

Serikali inasema kuwa wale waliokamatwa walikata kufika kuhojiwa Haki miliki ya picha AP/REUTERS
Image caption Serikali inasema kuwa wale waliokamatwa walikata kufika kuhojiwa

Viongozi wa chama cha upinzani nchini Uturuki kinachowaunga mkono wakurdi cha HDP, wamekamatwa pamoja na wabunge wengine 9.

Selahattin Demirtas na Figen Yuksekdag, wanalaumiwa kwa kueneza propaganda kwa niaba ya wanamgambo wanaopigana vita na taifa la Uturuki.

Saa chache baada ya bwana Demirtas kukamatwa eneo la Diyarbakir, mlipuko wa bomu uliwaua watu wanane na kuwajeruhi wengine zaidi ya 100.

Wanamgambo wamekuwa wakipigana vita kwa miaka mingi wakitaka kupata uhuru wa wakurdi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari lililipuka baada ya viongozi hao kukamatwa

Uturuki imesalia chini ya amri ya hali ya hatari ambayo ilitangazwa baada ya jaribio la mapinduzi lililotibuliwa mwezi Julai.

Amri hiyo inamruhusu Rais Recep Tayyip Erdogan na baraza lake la mawaziri kutotegemea bunge wakati wa kupitishwa sheria mpya na kuvuta uhuru wa watu.

Serikali inasema kuwa wale waliokamatwa walikata kufika kuhojiwa, ambapo pia waranti wa kukamatwa ulitolewa kwa wabunge wawili wa HDP ambao kwa sasa wako chi za ng'ambo.