Maandamano ya kumpinga rais wa Korea Kusini yafanyika Seoul

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Park Geun-hye amesema kashfa hiyo ilitokana na makosa yake

Maelfu ya raia wa Korea Kusini wamekusanyika kati kati mwa mji wa Seoul kufanya maandamao ya kumpinga Rais Park Geun-hye.

Wengi wanataka ajiuzulu kufuatia madai kuwa alimruhusu rafiki wake wa muda mrefu, kuwa na ushawishi kwenye masuala ya serikali.

Siku ya Ijumaa rais alitoa hotuba kwa njia ya televisheni akisema kuwa kashfa hiyo ilitokana na makosa yake.

Haki miliki ya picha AFP/GETTY
Image caption Bi Choi Soon-sil kwa sasa yuko korokoroni

Bi Park alijipata chini ya ushawishi wa mwanamke kwa jina Choi Soon-sil ambaye kwa sasa yuko kuzuizini.

Bi Choi anadaiwa kutumia fursa yake kunufaika kifedha