Msichana wa Chibok apatikana akiwa na mtoto Nigeria

Boko Haram hutumia wasichana hao kueneza propaganda Haki miliki ya picha AFP
Image caption Boko Haram hutumia wasichana hao kueneza propaganda

Mmoja wa wasichana wa chibok waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram nchini Nigeria, amepatikana akiwa na mtoto wa kiume wa umri wa miezi kumi kwa mujibu wa jeshi la nchi hiyo.

Msichana huyo alipatikana eneo la Pulkwa katika jimbo la Kaskazini la Borno.

Tangazo hilo lilitokea wiki tatu baada ya wasichana wengine 21 wa Chibok waliokolewa baada ya majadiliano na wanamgambo wa Boko Haram waliowateka.

Zaidi ya wasichana 270 wa shule walitekwa nyara kutoka mji ulio Kaskazini Mashariki mwa Nigeria mwaka 2014.

Boko Haram wamekuwa wakipigania kujitenga Kaskazini mwa Nigeria, kwenye mapigano ambayo yanakadiriwa kusababisha vifo vya watu 20,000.