M'marekani akiri kuwaua watu 7

Kohlhepp pia amewaonyesha polisi mahala alipowazika wahasiriwa wengine wawili katika makaazi yake.
Image caption Kohlhepp pia amewaonyesha polisi mahala alipowazika wahasiriwa wengine wawili katika makaazi yake.

Polisi katika jimbo la South Carolina wanasema mtu aliyekamatwa baada ya kisa ambapo mwanamke alipatikana amefungiwa ndani ya kasha nyumbani mwake,amekiri kuwaua watu saba.

Mtu huyo,Todd Kohlhepp amewaambia maafisa wa usalama wa jimbo hilo kwamba aliwapiga risasi na kuwaua watu wanne mwaka 2003.

Image caption Polisi walipelekwa hule ambapo jamaa huyo aliwuawa watu na kuwazika

Kohlhepp pia amewaonyesha polisi mahala alipowazika wahasiriwa wengine wawili katika makaazi yake.

Tayari polisi wamepata mwili wa mpenzi wa mwanamke aliyepatikana amefungiwa ndani ya kasha nyumbani kwake.