India yaionya Uingereza kuhusu sera ya uhamiaji

Idadi ya wanafunzi wa India katika vyuo vikuu vya Uingereza imepungua kwa asilimia hamsini katika kipindi cha miaka mitano itano iliyopita
Image caption Idadi ya wanafunzi wa India katika vyuo vikuu vya Uingereza imepungua kwa asilimia hamsini katika kipindi cha miaka mitano itano iliyopita

Maafisa wa India wameonya kuwa sera kali ya Uingereza juu ya Uhamiaji, dhidi ya wafanyikazi na wanafunzi wa India huenda ikaathiri biashara baina ya mataifa hayo mawili.

Onyo hilo linawadia huku waziri mkuu wa Uingereza Theresa May akitarajiwa kuzuru India kwa mazungumzo ya kutathmini uwezekano wa mataifa hayo kushirikiana kibiashara.

Msemaji wa serikali ya India mjini Delhi amesema idadi ya wanafunzi wa India katika vyuo vikuu vya Uingereza imepungua kwa asilimia hamsini katika kipindi cha miaka mitano itano iliyopita kutokana na sheria kali ya uhamiaji ambayo inawanyima nafasi ya kuendelea kuishi Uingereza baada ya masomo yao.

Bi May amesema atatumia ziara hiyo ya kibiashara ambayo ni ya kwanza tangu achaguliwa waziri mkuu kuimarisha biashara baina ya Uingereza na India kabla ya taifa lake kujiondoa rasmi kutoka muungano wa Ulaya.