Je,rais Magufuli ametimiza ahadi mwaka mmoja baadaye
Huwezi kusikiliza tena

Je,rais Magufuli ametimiza ahadi mwaka mmoja madarakani?

Rais John Magufuli wa Tanzania ametimiza mwaka mmoja tangu aingie madarakani. Wapo wengi wanaopendezwa na mtindo wa uongozi wake lakini, wakosoaji, japo wanafurahishwa na baadhi ya mambo, kuna mengine hawafurahishwi nayo. Kama sehemu ya maadhimisho yake, Rais Magufuli leo alikutana na waandishi wa habari Ikulu ya Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine amesema bado hajaridhishwa na mapambano dhidi ya rushwa, lakini anafurahishwa kwamba sasa nidhamu imeanza kurejea katika utumishi wa umma. Mwandishi wetu Sammy Awami amefanya tathmini ya mwaka mmoja wa serikali ya Rais Magufuli na kututumia taarifa hii.