Jacob Zuma : Siogopi kufungwa jela

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini
Image caption Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema kuwa haogopi kufungwa jela ,siku chache tu baada ya uchunguzi kubaini ushahidi kuhusu ufisadi katika serikali yake.

Hii ni mara ya kwanza kwa rais huyo kujitoa hadharani tangu ripoti moja ya ufisadi kutaka wanaohusika kushtakiwa.

Bwana Zuma mwenye umri wa miaka 74 anatuhumiwa na uhusiano mbaya na mfanyibiashara mmoja tajiri .

Amekana kufanya makosa yoyote.

Maelfu ya watu walifanya maandamano siku ya Jumatano wakimtaka Zuma ajiuzulu.

Ripoti hiyo yenye kurasa 355 iliangazia madai kwamba bwana Zuma aliiruhusu familia ya Gupta ilio karibu naye kushawishi uteuzi wa nyadhfa za baraza la mawaziri.

Ndugu hao wa Gupta hawajatoa tamko lolote ,lakini hapo awali wamekana kufanya makosa yoyote.