Operesheni ya kuukomboa mji wa Raqqa yaanza

Operesheni ya kuukomboa mji wa Raqqa yaanza
Image caption Operesheni ya kuukomboa mji wa Raqqa yaanza

Wapiganaji wanaosaidiwa na Marekani, kaskazini mwa Syria, wametangaza wanaanza operesheni ya kuukomboa mji wa Raqqa, shina la Islamic State nchini humo.

Wapiganaji hao ni wa kundi linalojiita wapiganaji wa demokrasi wa Syria, na watasaidiwa na ndege za kijeshi za Marekani.

SDF ni mkusanyiko Waarabu lakini wengi wao ni wapiganaji wa Kikurd.

Na wadadisi wanasema hilo linaweza kuwa tatizo.

Inadaiwa kuwa siku za nyuma, Wakurd waliwafukuza Waarabu kutoka miji fulani, na Wakurd wakisonga mbele hawatokaribishwa katika eneo la Raqqa , ambako watu wengi ni Waarabu.