Wapinzani waandamana Zimbabwe

Robert Mugabe
Image caption Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe

Polisi wa kutuliza ghasia nchini Zimbabwe wamerusha mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji wa upinzani katikati ya mji wa Zvishavane.

Chama cha Movement for Democratic Change kimetoa malalamiko kwamba polisi wamewatia mbaroni wafuasi wake licha ya amri ya mahakama kuruhusu maandamano hayo kuendelea.

Kumekua na maandamano katika miezi ya hivi karibuni nchini humo dhidi ya serikali ya Rais Robert Mugabe kutokana na kudorora kwa uchumi na kuanzishwa kwa mipango ya noti mpya.