Visima kumi na sita vya mafuta vyachomwa na IS Mosul

mosul
Image caption vikosi vya Iraq mjini Mosul

wanamgambo wa IS walioachia eneo la kusini ya Mosul nchini Iraq wamechoma moto visima vya mafuta kumi na tisa.

Mwandishi wa BBC kutoka eneo hilo anasema kuwa watu wengi wanaosumbuliwa na matatizo ya kupumua na wanyama wamekufa.

Uchafuzi wa mazingira kutokana na kuungua kwa visima hivyo vya mafuta kumesababisha mifugo kuwa na rangi nyeusi.

I-S bado wanadhibiti visima vya mafuta takribani sita nje ya Mosul na kuna hofu kwamba wanamgambo wake wanaweza kuchoma moto kwa visima hivyo pia.

Vikosi vya Serikali ya Iraq vimekua vikifanya jitihada katika siku za karibuni ili kukomboa mji wa Mosul kutoka kwa I-S.