Ni vyema kuweka picha za mwanao mtandaoni?

Mtoto akipigwa picha na mama yake Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Kizazi ambacho maisha yao yanaonyeshwa kwa kila mtu kwenye mitandao ya kijamii: Watataka kuyafuta wawapo watu wazima?

Wazazi kutoka Shanghai hadi Chicago wanajivunia kutuma picha za watoto watoto wao kwenye mitandao ya kijamii.

Huenda likachukuliwa kama jambo la kawaida, lakini hakuna watoto wa vizazi vya awali waliopata uzoefu huu wa kuwa kurekodiwa katika umma kwa maisha yao yote ya utoto kiasi hiki.

Nchini Uingereza, kwa wastani wazazi wenye mitandao ya kijamii wametuma picha 1,498 za watoto wao mtandaoini wakati wa mwaka wao wa tano wa kuzaliwa, kulingana na utafiti wa kampuni ya Nominet.

Hili huenda likawa hali halisi kote duniani miongoni mwa wazazi wanaojivunia kuwa wazazi - lakini vipi kuhusu watoto ambao walikuwa wadogo zaidi na hivyo kutokuwa na uwezo wa kuchagua.

Lakini watuwa kwanza kabisa kuweka picha za watoto wao kwenye mtandao sasa wamefikia umri wa utu uzima. Na si kwamba wakati wowote wanafurahia kutumwa kwa picha zao za utotoni kuhifadhiwa katika dijitali

"Nilipokuwa na umri wa miaka 12 ama 13 nilianza kutambua kuwa kulikuwa na vitu kwenye Facebook ambavyo nilidhani vilikuwa vya aibu kidogo," alisema Lucy mwenye umri wa miaka 16, kutoka Newcastle, ambaye baba yake amekuwa akituma picha zake kwenye mitandao ya kijamii tangu alipokuwa na umri wa miaka saba.

"Nilimuonmba aziondoshe na allifurahia pia, lakini hakuelewa ni kwanini. Kama ningeulizwa wakati huo, je ungependa picha hizi zitumwe kwa kila mtu azione, huenda ningesema hapana."

Haki miliki ya picha THINKSTOCK
Image caption Kote duniani maisha ya familia yanarekodiwa kupitia mitandao ya kijamii

Hata wale ambao waliridhishwa na kuwepo kwa picha zao kwenye mtandao wa kijamii kama watoto hawana uhakika kuhusu hilo sasa.

Dana Hurley, mwenye umri wa miaka 20, Kutoka mashariki mwa London, alisema kwamba kama msichana mwenye umri wa miaka 11 alifurahia sana kwa wazazi wake kutuma picha zake kwenye ukurasa wa Facebook.

"Wakati huo lilikuwa ni jambo la kusisimua… Napenda kutambuliwa. Sasa ni jambo la ajabu kiasi fulani , kwa sababu ukikumbuka nyuma na ufikirie, hii ilikuwa ni kwa ajili ya kila mtu kuangalia ,"alisema.

Aliondoa picha zake zote za utotoni kwenye mtandao, ikimaanisha kuwa picha hazionekani kwenye ukurasa wake, licha ya kwamba bado zipo kwenye mtandao.

Huenda wazazi wasitambue hili, lakini kwa kutuma picha na video za watoto wao kwenye mtandao, wanabuni utambulisho wa watoto wao ambao huenda usipendwe, kwamujibu wa mwanasaikolojia Dkt Arthur Cassidy, ambaye ni mtaalamu wa mitandao ya habari ya kijamii.