TB Joshua atabiri Bi Clinton atashinda urais Marekani

Muhubiri TB Joshua Haki miliki ya picha AFP
Image caption Muhubiri TB Joshua amesema kuwa Bi Clinton atashinda kwa ushindi mdogo dhidi ya mpinzani wake

Muhubiri maarufu wa vipindi vya Televisheni nchini Nigeria TB Joshua amesema ametabiri " kwamba Hillary Clinton atamshinda Donald Trump" katika uchaguzi wa urais wenye ushindani mkali tarehe 8 Novemba mwaka huu.

Katika ujumbe alioutuma kwenye ukurasa wake wa Facebook TB Joshua amesema kuwa Bi Clinton atashinda kwa ushindi mdogo, lakini atakabiliwa na changamoto nyingini - likiwemo jaribio la kupiga kwa kura ya kutokuwa na imani dhidi yake.

"boti ya rais mpya itakuwa imefungwa," aliongeza.

TB Joshua ni mmoja wa viongozi wa kidini wenye ushawishi na utata barani Afrika, huku wengi wa wafuasi wake wakiamini kuwa "utabiri " wake ni wa uhakika.