Wanawake waliosubiri miaka 96 kumpigia kura mwanamke

Wanawake waliopiga kura kwa njia ya posta Haki miliki ya picha I WAITED FOR 96 YEARS
Image caption Wanawake hawa, wote wakiwa na umri wa zaidi ya miaka 96, walipiga kura kwa njia ya posta na kupashana habari

Tarehe 8 Novemba, mamilioni ya wanawake wa kimarekani watafanya kile ambacho hawakupata fursa ya kukifanya kabla - kumpigia kura mwanamke aliyeteuliwa kama mgombea mkuu wa chama kuwa rais wa Marekani.

Kwa baadhi yao hii kikomo cha miaka 96 ya kusubiri.

Yeyote aliyezaliwa kabla ya tarehe 18 Augusti 1920 nchini Marekani alianza maisha katika nchi ambayo haikumruhusu wanawake kupiga kura.

Hao ni pamoja na Estelle Schultz, mwenye umri wa miaka 98, aliyekuwa akifanya kazi kwenye viwanda viwili katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia na mwalimu wa muda mrefu,ambaye alipelekwa kwenye kituo cha kupigia kura kama mtoto na mama yake kushuhudia namna kura zinavyopigwa.

Estelle ana matatizo makubwa ya moyo na yuko chini ya uangalizi wa hospitali. Lakini anasema: "nimeamua kwamba ningependa kuishi muda mrefu wa kutosha kuweza kushudia kuchaguliwa kwa mwanamke wetu wa kwanza rais ."

Haki miliki ya picha SARAH BENOR
Image caption Ninatuma hii kwa ombi la bibi yangu mwenye umri wa miaka 98, ambaye hatumii kompyuta ,' aliandika Sarah

Mwezi Oktoba, alipokuwa akipiga kura yake ya awali kwa njia ya posta, alisema kuwa alibaini ni kiwango gani hali hiyo "ilivyo muathiri" , na akamuomba mjukuu wake wa kike Sarah kutuma picha yake hii kwenye Facebook

Picha hii ilipendwa na mamia ya watu kwa ishara ya ''like'', suala lililoibua shauku ya sara na familia yake kutafuta taarifa zinazofanana na ya bibi yao.

Waliwapata wengine wengi, na wavuti " Nilisubiri miaka 96 " ulianzishwa, na kujaa kauli kutoka kwa wafuasi wa Hillary Clinton waliozaliwa kabla wanawake kuwa na haki ya kupiga kura.

Baadhi ni watu wazima wa kutosha kiasi cha kukumbuka wakati wanawake walipopewa fursa ya kupiga kura, mara baada ya kuidhinishwa kwa marekebisho ya 19 ya katiba ya Marekani.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mfuasi wa Democrat mwenye umri wa miaka 102 "Jerry" Emmett pia ni mchangiaji wa tovuti

"nakumbuka nikimsindikiza mama yangu tukiwa kwenye farasi kuelekea kwenye kituo cha kupigia kura katika uchaguzi wa kwanza ambapo wanawake waliruhusiwa kupiga kura. Hatimae baada ya muda mrefu nilikuwa na haki ya kupiga kura ,"aliandika Juliet Bernstein mwenye umri wa miaka 103 kutoka Massachusetts, ambaye alizaliwa mwaka 1913, na kupaya shahada ya kwanza kwa kutiwa hamasa na mama yake.

Mama yangu alikuwa miongoni mwa wanawake wa kwanza kukata nywele zao kuwa fupi na kubadilisha mtindo wa sketi ndefu zilizokuwa zikiburuzwa kwenye matope na kuvaa magauni mafupi ," alisema Beatrice Lumpkin, mwenye miaka 98, kutoka Chicago.

"yote ni juu ya haki zetu , wakianza na haki yao ya kupiga kura. Nilipokuwa mtu mzima kiasi cha kuelewa ni vipi wapigania haki ya kupiga kura nilijivunia sana''

Baadhi ya wachangiaji wa mtandao huo wanasema wanayo furaha kuwa na fursa ya kumpigia kura mwanamke kama raia katika kipindi cha uhai wao - kitu ambacho wengi hawakudhani kingewezekana.