Mambo muhimu kuhusu uchaguzi mkuu Marekani
Huwezi kusikiliza tena

Mambo muhimu kuhusu uchaguzi mkuu Marekani

Imekuwa kampeni kali. Hillary Clinton na Donald Trump wote wamehitajika kujitetea dhidi ya tuhuma mbalimbali. Wiki za mwisho zimekuwa ngumu kwa wote wawili - lakini kila mmoja ana kundi la wafuasi waaminifu, sasa wanapigania kura dakika za mwisho.

Siku ya uchaguzi, mshindi si lazima awe yule anayepata kura nyingi kwa jumla. Kuna majimbo 50 na Washington D.C. Kila jimbo huwa na 'Kura za Wajumbe' kwa kutegemea sana wingi wa watu.