Nguo ya ndani ya mke wa Hitler yapigwa mnada

Suruali ya ndani ya mkewe Adolf Hitler imepigwa mnada Haki miliki ya picha PHILLIP SERREL
Image caption Suruali ya ndani ya mkewe Adolf Hitler imepigwa mnada

Nguo ya ndani ya mke wa Adolf Hitler Eva Braun imeuzwa katika mnada kwa pauni 3000.

Suruali hiyo ikiwa ni miongoni mwa vitu vyengine vya bi. Braun ilipigwa mnada katika jumba la mnada la Phillip Serrell huko Melvern ,ikitarajiwa kuvutia pauni 400 lakini ikauzwa kwa pauni 2,900.

Pete ya dhahabu na kiboksi chenye kioo kilichokuwa na lipstiki nyekundu ya Eva Braun pia kiliuzwa.Vyote hivyo viliuzwa kwa mtu binafsi.

Haki miliki ya picha Phillip Serrel
Image caption Vito vya Eva Braun

Suruali hiyo ilikuwa na kamba ilikuwa na mapambo ya herufi za Eva Braun.

Pete ya dhahabu iliozungukwa na madini iliuzwa kwa pauni 1,250 huku lipstiki hiyo ya rangi ya fedha ikiuzwa kwa pauni 360.

Wakati huohuo picha za rangi nyeupe na nyeusi za Eva Braun na Adolf Hitler ziliuzwa kwa pauni 100.

Haki miliki ya picha Phillip Serrel
Image caption Picha nyeusi na nyeupe ya Eva Braun

Wanaoendesha mnada huo wamethibitisha kuwa ziliuzwa kwa mtu binafsi kutoka Uingereza.