Mpiga mbizi aliyepata bomu la nyuklia?

Bomu la nyuklia lililopotea
Image caption Bomu la nyuklia lililopotea

Mpiga mbizi mmoja huenda amegundua bomu la kinyuklia la Marekani ambalo lilipotea katika pwani ya Canada.

Sean Smyrichinsk alikuwa akiogelea akiwatafuta majongoo wa baharini karibu na Colombia inayomilikiwa na Uingereza wakati alipogundua chuma kikubwa kilicho fanana na kisahani .

Idara ya ulinzi nchini Canada inaamini huenda ni bomu la kinyuklia kutoka kwa ndege ya kivita aina ya US B-36 Bomber ilioanguka katika eneo hilo 1950.

Serikali hiyo haiamini kwamba bomu hilo lina Nyuklia.

Canada tayari imetuma ndege ya wanamaji katika eneo hilo karibu na Haida Gwaii ili kulikagua bomu hilo.