Panama kuwakabili Marsh Academy Ligi ya wanawake

jkt Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Wachezaji wa kikosi cha Jkt Queens

Raundi ya Pili ya Duru la Kwanza ya Ligi Kuu ya Taifa ya Wanawake itaendelea leo kwa mchezo mmoja tu, Panama ya Iringa watakua wageni wa timu ya Marsh Academy kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Michezo mingine mitano ya raundi ya pili ikiwamo mitatu ya Kundi A, imebidi iahirishwe na itapangiwa tarehe nyingine. Sababu kubwa ya kuahirishwa kwa michezo hiyo ni uwingi wa wachezaji kutoka timu zinazoshiriki ligi hiyo kujumuishwa kwenye timu ya taifa ya Wanawake - Twiga Stars.

Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo, michezo ya Kundi B iliyoahirishwa ni kati ya Majengo Women ya Singida iliyokuwa icheza na Baobab ya Dodoma.

Huku Victoria Queens ya Kegera iliyokuwa icheze na Sisters ya Kigoma - mchezo ulipangwa kufanyika Uwanja wa Katiba mjini Bukoba.

Michezo ya Kundi A iliyoahirishwa ni kati ya Fair Play ya Tanga iliyokuwa iikaribishe Mburahati Queens ya Dar es Salaam

JKT Queens ya Dar es Salaam ilikuwa icheze na Viva Queens kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakati Evergreen Queens na Mlandizi zilikuwa zitumie Uwanja wa Karume, Ilala kucheza mechi yao hiyo.