Ronaldo: Bado nina miaka kumi ya kucheza soka

Ronaldo Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Cristiano Ronaldo baada ya kusaini mkataba mpya

Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amesema anaweza kuendelea kucheza soka kwa miaka kumi zaidi baada ya kusaini mkataba mpya na klabu yake.

Ronaldo Mwenye umri wa miaka 31 mkabata wake ulikua unamalizika mwezi Juni 2018, lakini mkataba mpya aliosaini utamuweka kwa miamba hao wa soka wa Hispania mpaka Juni 2021.

Mchezaji huyu amesema "Nilichokua nakitaka ni kuendelea kufurahia kucheza kwa miaka iliyobaki. na bado nina miaka kumi,"

Nyota huyu amefunga mabao 371, toka alipojiunga na Real Madrid akitokea Manchester United, mwaka 2009.

Ronaldo ameisaidia Real Madrid, kutwaa ubingwa wa ulaya mara mbili, ubingwa wa la Liga na mataji mengine.