Nigeria:polisi wa kike kulinda waathiriwa wa Boko Haram

Maiduguri Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Zaidi ya watu 16,000 wanaishi katika kambi ya Maiduguri nchini Nigeria

Mamlaka nchini Nigeria zimesema kuwa kupelekwa kwa maafisa wa polisi wa kike katika kambi kaskazini-mashariki ya nchi hiyo kutasaidia wanawake waathiriwa wa Boko Haram kujisikia salama zaidi.

kamishna wa Polisi Damian Chunkwu amesema kuwa polisi wa kike watahakikisha ulinzi wa wanawake katika kambi.

wanaharakati wa haki za binadamu wametuhumu vikosi vya usalama kwa kudhalilisha wanawake kingono katika kambi hizo.

Rais Buhari ameagiza uchunguzi kufanyika juu ya madai hayo. Maafisa mia moja wa polisi wa kike wamepelekwa katika kambi hizo.